UTT AMIS ilianzishwamwaka 2013 kuchukua majukumu ya usimamizi wa Mifuko ya Uwekezaji wa pamoja kutoka kwa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) kufuatia maamuzi ya wamiliki kubadilisha muundo. Kampuni ya UTT AMIS inasimamia Mifuko sita ya uwekezaji wa pamoja ambayo ni Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu, Mfuko wa Ukwasi na Mfuko wa Hati Fungani. Zaidi yahayo, UTT AMIS inatoa huduma ya usimamizi mali za kifedha kukidhi mahitaji maalum kwa wawekezaji binafsi wa kipato cha kati na cha juu pamoja na taasisi. UTT AMIS inaendeshwa na Bodi ya Wakurugenzi inayoundwa na wataalamu wenye taaluma mbalimbali na uzoefu kwenye soko la fedha na mitaji.
UTT AMIS, hapo awali ilijulikana kama Dhamana ya uwekezaji Tanzania (UTT) ambayo ilianzishwa chini ya Sheria ya Udhamini (SheriayaDhamana Na. 318) na kupewa majukumu kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na Kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja katika njia ambayo itaongeza thamani ya mifuko hiyo, kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba kupitia ushiriki mpana katika umiliki wa vipande. UTT AMIS imefanikiwa kuvutia zaidi ya wawekezaji 150,000 kutoka nchi nzima na pia wamekuwa wasimamizi bora wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja Tanzania.
Kwa muda wote tangu kuanzishwa Taasisi ya UTT AMIS imekua kinara na msaada kwenye jukwaa la uwekezaji. UTT AMIS ina rekodi nzuri ya ufanisi kwenye Nyanja ya uwekezaji na ilitunukiwa tunu ya kuwa msimamizi bora wa Mifuko nchini Tanzania kwa Mwaka 2015 na Jumuiya ya Fedha ya Kimataifa ya Uingereza. (Capital Finance International of UK).