Mkurugenzi Mtendaji
Bwana Simon Migangala ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS. Bwana Migangala ana shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara na fedha (MBA) kutoka chuo cha IMD, Lausanne nchini Switzerland, Shahada ya kwanza ya uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, pamoja na shahada ya juu ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu, CPA (T) iliyotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA), Cheti kutoka Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana.
Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara
Bwana Wahichinenda ni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Maendeleo ya Biashara, ana shahada ya kwanza ya Sanaa katika takwimu na pia ana shahada ya uzamili ya sayansi katika masuala ya fedha aliyoipata kutoka katika chuo kikuu cha Strathclyde, Glasgow, Scotland.
Mkurugenzi wa Uwekezaji
Bibi Pamela ni Mkurugenzi wa Uwekezaji, ana shahada ya uzamili katika utawala wa biashara kutoka ESAMI na pia anashahada ya kwanza ya biashara kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Bibi Pamela pia amehudhuria kozi mbalimbali ikiwemo mshauri katika mambo ya uwekezaji kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na amethibitishwa katika kufanya kazi mbalimbali katika soko la hisa la Dar es salaam pamoja na soko la bidhaa (commodity Exchange).
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma na Masoko
Bwana Mbaga ni mkuu wa kitengo cha mahusiano ya Umma na Masoko akihusika na kutengeneza mipango na utekelezaji wa mikakati ya masoko, mauzo, mahusiano pamoja na mawasiliano kwa umma. Bwana Mbaga alijiunga na UTT AMIS mwaka 2003 kama mkurugenzi wa masoko akiwa na uzoefu wa miaka zaidi ya ishirini alioupata katika kampuni ya Shirika la viwango Tanzania, DHL, National Media Group pamoja na Protrade.
Mkurugenzi wa Huduma za Kampuni
Bibi Joan ni Mkurugenzi wa Huduma za Kampuni anaye shughulikia masuala yote ya Fedha, Uhasibu katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja, Rasilimali watu pamoja na Utawala. Bibi Joan alijiunga na UTT AMIS mwaka 2013 kama afisa mwandamizi wa fedha kabla ya kupandishwa cheo na kuwa mkurugenzi wa fedha na utawala (kwa sasa mkurugenzi wa huduma za kampuni).
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Takwimu.
Bibi Sophia Mgaya ni mkuu wa kitengo cha Technolojia ya Habari, mawasiliano na Takwimu anayehusika na kutengeneza sera na miongozo ya Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Takwimu na kusimamia utekelezaji wake. Pia anahusika na kuweka mifumo mbalimbali ambayo itarahisisha utendaji kazi nautunzaji wa taarifa muhimu za kampuni ikiwemo wawekezaji.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi
Bwana Bujiku ni Mkuu wa kitengo cha ununuzi anayeshughulika na mambo yote ya ununuzi katika kampuni ya UTT AMIS. Bwana Bujiku ni Mtaalamu mwenye shahada ya juu ya Ununuzi (CPSP) iliyotolewa na Bodi ya Ununuzi Tanzania (PSPTB), ana shahada ya juu ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (CPA) iliyotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA).
Head of Legal Services Unit

Tuzo is the Head of Legal Services Unit for UTT AMIS. She joined UTT AMIS in May 2019. Tuzo is responsible for controlling and managing Legal affairs of the company.

Director of Human Resource and Administration

Kaniki is the Director of Human Resource an Administration. He is responsible for overseeing all matters related to Coordination, Administration and Human Resource in the organization.