Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Takwimu.

Bibi Sophia Mgaya ni mkuu wa kitengo cha Technolojia ya Habari, mawasiliano na Takwimu anayehusika na kutengeneza sera na miongozo ya Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Takwimu na kusimamia utekelezaji wake. Pia anahusika na kuweka mifumo mbalimbali ambayo itarahisisha utendaji kazi nautunzaji wa taarifa muhimu za kampuni ikiwemo wawekezaji. Bibi Mgaya alijiunga na UTT AMIS mwaka 2007 na kuanzia kipindi hicho amefanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ya huduma kwa wateja kwa njia ya simu, na kuunganisha mifumo ya kampuni ya UTT AMIS na benki washirika pamoja na kampuni za simu. Kabla ya kujiunga na UTT AMIS, Bibi Sophia alifanya kazi katika Wizara ya Ardhi pamoja na Shirika la Posta Tanzania. Bibi Sophia ana shahada ya uzamili ya utawala wa biashara toka ESAMI, stashahada ya Uzamili ya TEHAMA kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Stashahada ya Juu ya Teknolojia ya Habari kutoka Chuo cha usimamizi wa fedha (IFM).