Mkurugenzi Mtendaji

Bwana Simon Migangala ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTT AMIS. Bwana Migangala ana shahada ya Uzamili katika Utawala wa Biashara na fedha (MBA) kutoka chuo cha IMD, Lausanne nchini Switzerland, Shahada ya kwanza ya uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, pamoja na shahada ya juu ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu, CPA (T) iliyotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA), Cheti kutoka Mamlaka ya masoko ya Mitaji na Dhamana. Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji, Bwana Migangala alihudumu katika nafasi ya Afisa Mwendeshaji Mkuu katika Kampuni ya UTT AMIS akiwajibika katika kusimamia utendaji wa kurugenzi za Fedha na Utawala, Uwekezaji, Uendeshaji, Masoko na Uhusiano wa Umma pamoja na Kurugenzi ya

Tehama. Bwana Migangala pia alisimamia zoezi la utayarishaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Kampuni ya UTT AMIS ambao uliwezesha uwekezaji kukua kutoka bilioni 178 mpaka bilioni 300.Kablaya Kujiunga na kampuni ya UTT AMIS, Bwana Migangala alifanya kazi kama mshauri wa kujitegemea katika Nyanja za fedha na shughuli za benki kwa kipindi cha miaka mitatu na pia alihudumu katika nafasi ya ukurugenzi akisimamia uwekezaji, masoko ya fedha, fedha za kigeni pamoja na bidhaa zote za soko la Mitaji na Dhamana katika benki ya CRDB. Bwana Migangala pia alifanya kazi na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi, PricewaterhouseCoopers kama mkaguzi.