Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi

Bwana Bujiku ni Mkuu wa kitengo cha ununuzi anayeshughulika na mambo yote ya ununuzi katika kampuni ya UTT AMIS. Bwana Bujiku ni Mtaalamu mwenye shahada ya juu ya Ununuzi (CPSP) iliyotolewa na Bodi ya Ununuzi Tanzania (PSPTB), ana shahada ya juu ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu (CPA) iliyotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA). Bwana Bujiku alipata shahada ya Biashara kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 1995 na baada ya hapo alipata stashahada ya rasilimali watu, Stashahada ya Uzamili katika masuala ya ununuzi na usimamizi wa ugavi kutoka chuo cha usafirishaji Dar es salaam,pia alipata Astashahada ya kimataifa, Astashahada ya juu ya kimataifa na stashahada ya kimataifa katika maswala ya usimamizi wa ugavi na usimamizi wa mnyororo wa thamani kutoka Kituo cha Biashara cha kimataifa (ICT). Kwa sasa bwana Bujiku ni mtahiniwa katika fani ya uchambuzi wa masuala ya fedha (Chartered Financial Analyst). Bwana Bujiku alijiunga na UTT AMIS kama Afisa mwandamizi wa fedha mwaka 2006 kutokea kampuni ya Audit Control and Expertise ambako alihudumu kama Meneja wa fedha na Utawala. Bwana Bujiku alifanya kazi na kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa hesabu, Coopers and Lybrand /PricewaterhouseCoopers kwa kipindi cha miaka sita.