Bwana Mbaga ni mkuu wa kitengo cha mahusiano ya Umma na Masoko akihusika na kutengeneza mipango na utekelezaji wa mikakati ya masoko, mauzo, mahusiano pamoja na mawasiliano kwa umma. Bwana Mbaga alijiunga na UTT AMIS mwaka 2003 kama mkurugenzi wa masoko akiwa na uzoefu wa miaka zaidi ya ishirini alioupata katika kampuni ya Shirika la viwango Tanzania, DHL, National Media Group pamoja na Protrade. Bwana Mbaga ana shahada ya uzamili katika utawala wa biashara kutoka chuo kikuu cha Mzumbe pamoja na shahada ya kwanza ya biashara kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam. Bwana Mbaga amehudhuria kozi mbalimbali za muda mfupi katika Nyanja za masoko ndani na nje ya nchi
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma na Masoko