Mjumbe wa Bodi

Dokta Mohamed ni Mhadhiri mwandamizi katika masuala ya fedha katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Dokta Mohamed ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, Glascow, Scotland. Dokta Mohamed amehudhuria kozi mbalimbali za muda mfupi ikiwemo kozi katika masoko ya fedha. Pia ameshiriki kufanya tafiti mbalimbali katika Nyanja za uwekezaji, uchumi na kutoa ushauri katika masuala ya kifedha na kibenki pamoja na uongozi/utawala katika Makampuni/ Mashirika naTaasisi, kazi ambazo amezifanya kwa zaidi ya miaka thelathini.