Mfuko wa Umoja ni mfuko wa wazi wenye uwiano sawa wa uwekezaji unaoufanya kuwa mfuko bora wenye hatari za uwekezaji wa kiwango cha kati. Mfuko wa Umoja unawekeza kiwango kisichozidi asilimia 50 ya fedha zake kwenye hisa zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es salaam na asilimia 50 nyingine huwekezwa kwenye masoko mengine ya fedha na mitaji yenye sifa tofauti.

Sera ya uwekezaji kwa upande mmoja ni mpango madhubuti uliowekwa na mfuko ili  kutawanya rasilimali zake. Kwa upande mwingine ni mpango mkakati na ni kinga endapo eneo moja la uwekezaji likifanya vibaya. Aidha, uwekezaji kwenye hisa huwekezwa kwa kiwango cha chini ikilinganishwa na eneo lenye mapato cha kudumu (Fixed Income).

Ni mfuko wa kwanza kuanzishwa na umekuwa sokoni tangu mwezi wa tano mwaka 2005. Kwasasa mfuko unathamani inayozidi billioni 213 na wawekezaji zaidi ya 95,000.

Kwa muda mrefu sasa mfuko umekuwa ukitoa faida nzuri iliyo kati ya asilimia 10 mpaka 20 (ukitoakodi).

Mwekezaji wa mfuko wa Umoja anaweza kuuza vipande vyake muda wowote, pesa ataipata ndani ya siku kumi za kazi toka alipowasilisha maombi. Hakuna kipindi cha kizuizi.

Gharama za kuuza vipande vya mfuko ni asilimia 1 ya thamani ya kipande ambayo ni nafuu zaidi sokoni kwa kulinganisha na asilimia 10 ya kodi atakayokatwa mteja anayetoa fedha zake alizoweka kwenye akiba ya muda maalumu ya benki.

Tathmini ya thamani halisi ya Mfuko itakokotolewa kila siku ya kazi na thamani ya kipande kutangazwa.

Usalama wa fedha za mwekezaji ni mkubwa kwasababu mfuko unasimamiwa na taasisi ya serikali yenye kuaminika. Pia mfuko unatoa faida shindani,ukwasi na usalama kwa fedha za mwekezaji.

Kwa kuzingatia maelezo hayo, unaweza kuwekeza kiwango cha kawaida kabisa katika mfuko wa UMOJA na utawezeshwa kufuatilia maendeleo yake kwa ukaribu.