Madhumuni: Mfuko huu ni mpango ulio wazi unaotoa njia nyingine ya uwekezaji kwa wawekezaji wanaotaka kuweka fedha zao kwa kipindi cha muda mfupi na katika kiwango kilichopo kwenye ushindani. Hatari/Athari kidogo katika uwekezaji na ukwasi wa hali ya juu ndio dhumuni hasa la mfuko huu.

Sera ya Uwekezaji: Kiwango cha chini cha uwekezaji katika masoko ya fedha itakuwa asilimia hamsini (50%) na fedha inayobaki itawekezwa katika Dhamana.

Chaguo la mpango wa Uwekezaji: Mfuko huu unatoa fursa ya uwekezaji unaokua pamoja na kujitoa katika uwekezaji pasipo na gharama yoyote

Nani anaruhusiwa kuwekeza: Mfuko uko wazi kwa mtanzania aliye ndani au nje ya nchi, inahusisha watu binafsi (ikijumuisha watoto), na wawekezaji wasio watu binafsi kama Mifuko ya Pensheni, Mabenki/Mashirika Taasisi za serikali, Vyombo vya ulinzi na usalama, Asasi zisizo za kiserikali na Mashirika mengineyo n.k

Kiwango cha chini cha uwekezaji: a) Uwekezaji wa mwanzo= Shs 100,000 (b) Mauzo yanayofuata = Shs 10,000

Kiwango cha juu cha uwekezaji: Hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza.

Umiliki wa Vipande: Umiliki wa mtu mmoja na umiliki wa pamoja unaruhusiwa katika mfuko huu. Hata hivyo, umiliki wa pamoja hauzihusu taasisi/kampuni.

Ukwasi: Baada ya kipindi cha utulivu kumalizika, uuzaji wa vipande utafanyika kila siku ya kazi. Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) itatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya masaa 24 baada ya kupokea fomu za maombi katika Makao Makuu ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania. Fedha za mauzo zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji.

Tozo la kujiunga na kujitoa: Mwekezaji hatotozwa gharama yeyote ya kujiunga au kujitoa katika mfuko

Kigezo: Dhamana za Serikali za siku 35

Ulinzi wa mtaji: Lengo kuu ni kulinda mtawanyo wa uwekezaji ili kutoathili thamani ya vipande huku mtazamo mkuu ukiwa ni kipato kinachotokana na riba bila hatari zisizokuwa na ulazima.