MFUKO WA JIKIMU

Madhumuni:Mfuko huu ni mpango uliowazi wenye lengo la kukuza na kutoa gawio kutokana na mapato ya ziada katika vipindi tofauti na pia kukuza mtaji kwa mwekezaji wa muda mrefu.

Chaguo la Mpango wa Uwekezaji:

Mfuko unatoa fursa mbili za uwekezaji- (a)Mapato ya robo mwaka (b)Mapato ya mwaka yaliyoambatanishwa na ukuaji wa vipande (growthoption)

Nani anaruhusiwa kuwekeza:Mfuko uko wazi kwa watanzania waliondani na nje ya nchi, watu binafsi,makampuni / taasisi,mabenki,asasizakiraia(NGO)n.k. kama inavyoonyeshwa kwenyewaraka huu.

Kiwango cha Chini cha Kuwekeza:Ni Shilingi (Sh.) milioni 2 kwa mpango wa mapato ya robo mwaka, na Shilingi milioni moja kwa mpango wa gawio kwa mwaka na Sh.5,000 kwa mpango wa ukuaji wamtaji kwa mwaka.

Uwekezaji wa Nyongeza: Kiwango cha chini cha uwekezaji wa nyongeza/unaofuata (additionalinvestment) ni Sh.15,000 kwa mpango wowote wa gawio na Sh.5,000 kwampango wa ukuaji wa mtaji kwa mwaka, hakuna ukomo wa kiwango cha kuwekeza

Makato ya Kodi:Kulingana na sheria za sasa,kodi ya mapato haitotozwa kwenye gawio litokanalo na uwekezaji kwenye mfuko huu.

Uhamishaji wa Vipande: Uhamishaji wa vipande kutoka kwenye mfuko mmoja kwenda mwingine kati ya mifuko inayoendeshwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania unaruhusiwa. Uhamishaji huu utatumia thamani halisi ya kipande kwa wakati huo bila gharama yoyote. Uhamishaji huo utafanywa kwa mauzo ya vipande kutoka kwenye mfuko mmoja na kuviwekeza kwa kununua vipande kwenye mfuko mwingine, ilimradi sifa za kuwekeza kwenye mfuko mwingine zimezingatiwa.