Mwenyekiti wa Bodi
Bwana Casimir S. Kyuki kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya UTT AMIS, pia ni Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
Mjumbe wa Bodi
Bwana Juma A. Muhimbi ni Mjumbe wa Bodi ya UTT AMIS, pia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya IMMA Consultancy Services Ltd. Bwana Muhimbi ana Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Nyanja za Uhasibu na Fedha aliyoipata kutoka chuo kikuu cha Birmingham cha nchini Uingereza na pia ni Mhasibu na Mkaguzi aliyethibitishwa na Bodi ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) akiwa na shahada ya juu, CPA (T) inayotolewa na bodi hiyo.
Mjumbe wa Bodi
Dokta Mohamed ni Mhadhiri mwandamizi katika masuala ya fedha katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Dokta Mohamed ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde, Glascow, Scotland. Dokta Mohamed amehudhuria kozi mbalimbali za muda mfupi ikiwemo kozi katika masoko ya fedha. Pia ameshiriki kufanya tafiti mbalimbali katika Nyanja za uwekezaji.
Mjumbe wa Bodi
Bwana Hamisi ana shahada ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam pamoja na stashahada ya uzamili katika maendeleo ya kiuchumi kutoka taasisi ya maendeleo ya kiuchumi (IDEP) nchini Senegal. Bwana Hamisi anauzoefu wa muda mrefu kutoka wizara ya Mipango na Uchumi.
Mjumbe wa Bodi
Bwana Chachah ni Afisa Usimamizi wa Fedha na Mtaalamu wa masuala ya Ununuzi Wizara ya Fedha na Mipango katika kitengo cha uchambuzi wa Sera. Bwana Chachah anauzoefu wa zaidi ya miaka Ishirini katika masuala ya usimamizi wa fedha.