Mkutano wa mwaka (AGM) kwa wawekezaji wa Mifuko ya uwekezaji wa pamoja

 ulifanyika kuanzia tarehe 31 Novemba 2019 hadi  01 Desemba 2019 Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam. Mkutano ulitoa mrejesho wa taarifa za mifuko na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye uwekezaji wa pamoja wa mifuko ya Umoja, Wekeza Maisha, Watoto, Jikimu na Ukwasi. Mfuko mpiya wa 'Bond Fund' pia ulizinduliwa.

Wawekezaji walifahamishwa kurahisishwa kwa huduma za kununua vipande kwa njia ya simu kwa kupitia UTT AMIS shortcode namba *150*82# , UTT AMIS App na mitandao ya simu ya Tigo, Vodacom, Airtell, Halotell. Wawekezaji pia walifahamishwa wanaweza kununua vipande moja kwa moja kupitia chaneli za CRDB kama vile CRDB App, Fahali Huduma na nyinginezo.