Kampuni ya Uwekezaji ya UTTAMIS inashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ndani ya banda la Wizara ya Fedha na Mipango. Katika maonyesho hayo wananchi wanaotembelea banda wataweza kupata maelezo mbali mbali kuhusu uwekezaji unaofanywa na taasisi hiyo kupitia mifuko yake ya Uwekezaji wa Pamoja.
 

Taasisi hii kwa takribani muongo mmoja imekuwa ikitoa huduma za Uwekezaji kwenye masoko ya fedha na mitaji hivyo kuwawezesha wananchi kushiriki kwenye masoko hayo bila wao wenyewe kwenda moja kwa moja kwa madalali wa soko la hisa.
 

Wawekezaji waliotembelea banda hili wamekuwa na mwitikio chanya kutokana na huduma zitolewazo na taasisi hii kwa kupata faida shindani kwenye soko na kuongeza thamani ya pesa zao huku taasisi ikihakikisha ukwasi wa hali ya juu kwa wawekezaji wanaohitaji pesa zao.

Kwa sasa taasisi hii imerahisisha huduma kwa kuanzisha uwekezaji kwa njia ya simu yaani UTT SIMINVEST ambapo mwekezaji mpya anaweza kufungua akaunti ili kujiunga na mifuko ya uwekezaji.Vile vile kupitia huduma hii ya uwkezaji kiganjani wawekezaji ambao wameshajiunga wanaweza kutembelea banda la UTTAMIS ili kujaza fomu za kujiunga na huduma hii ili waweze kupata thamani ya vipande,Taarifa fupi,Kuuliza salio na kununua vipande.