
Mfuko wa Wekeza Maisha ni mfuko wa kwanza wa uwekezaji wa pamoja kuanzishwa na kampuni ya UTT AMIS nchini wenye faida za bima ya maisha ndani yake.
- Faida za Bima ya maisha
- Faida za uwekezaji wa muda mrefu.
Zaidi yaasilimia 99 za fedha za wawekezaji wa mfuko wa Wekeza Maisha huwekezwa kwenye masoko mbalimbali ya fedha na asilimia 1 kwa ajili ya malipo ya bima.
MAMBO MUHIMU KUHUSU MFUKO WA WEKEZA MAISHA
- Madhumuni: Mfuko huu ni mpango wa wazi na wa muda mrefu unaokusudia kukuza mtaji na kwa wakati huo huo kutoa kinga ya Bima ya Maisha, Bima ya Ajali/Ulemavu wa Kudumu na Gharama za Mazishi.
- Chaguo la Mpango wa Uwekezaji: Mfuko unatoa fursa mbili za uwekezaji: (a) Mpango wa Uwekezaji kwa Awamu (Regular Contribution) na (b) Uwekezaji wa Mkupuo (Single Contribution).
- Nani anaruhusiwa Kuwekeza: Mfuko uko wazi kwa Mtanzania aliye ndani au nje ya nchi na awe mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 55.
- Ukomo wa Uwekezaji: Uanachama wa mwekezaji katika mfuko huu utakoma baada ya miaka 10.
- Ukwasi: Uuzaji wa sehemu ya uwekezaji (vipande) katika mfuko (Partial Repurchase) unaruhusiwa baada ya miaka mitano (5)
- Thamani ya Mwanzo ya Kipande: Thamani ya mwanzo ya Kipande (face value) ilikuwa Sh.100/=
- Bei ya Kipande: Bei ya Kipande wakati wa mauzo ya mwanzo, yaani kuanzia tarehe 16 Mei, 2007 hadi Julai 31, 2007 ilikuwa ni Sh.100/= na baada ya hapo Kipande kinauzwa kulingana na thamani halisi.
- Kiwango cha Kuwekeza: (a) Kiwango cha chini kwa uwekezaji kwa miaka kumi ni Sh. Milioni 1 na (b) Hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza (isipokuwa mafao ya Bima ya Maisha yatatolewa mpaka kufikia kiwango cha Sh. Milioni 25 tu). Milioni hii moja inaweza kuwekezwa kwa awamu au kwa mkupuo. Kiwango cha chini cha uwekezaji wa awamu ni Sh.8,340/= kwa kila mwezi.
- Mafao ya Bima ya Maisha – Kifo au Ulemavu wa Kudumu (Death or Total and Permanent Disability);
- Mpango wa kuwekeza kwa Awamu: Kinga ya Bima ya maisha ina thamani sawa na kiasi kisicholipwa na mwekezaji kwa muda uliosalia katika mpango wake wa uwekezaji. (Muhimu: Kiwango cha juu kulipwa ni Sh. Milioni 25).
- Mpango wa Kuwekeza kwa Mkupuo: Kinga ya Bima ya Maisha ina thamani sawa na kiwango alichochagua mwekezaji. (Muhimu: Kiwango cha juu cha kulipwa ni Sh. Milioni 25).
- Mafao ya Bima ya Ajali: Mwekezaji atalipwa asilimia 20 ya kiwango kilichokusudiwa katika mpango wa uwekezaji, hata hivyo kiwango cha juu ni Sh. Milioni 5 tu.
- Mafao ya Gharama za Mazishi: Kila mwekezaji atalipwa Sh.500,000/= kwa ajili ya mazishi endapo atafariki bila kujali kiwango alichowekeza. Mafao haya yatalipwa kwa ajili ya wawekezaji watakaoingia wakati wa mauzo ya mwanzo tu.
- Mkono wa Pongezi (Loyalty Bonus): Mfuko utatoa mkono wa pongezi kwa mwekezaji ambaye atakamilisha miaka kumi ya mpango wake wa uwekezaji au kama atafariki ndani ya mwaka wa mwisho wa mpango wake wa uwekezaji.